MSANII WA HIPHOP 'WAKAZI' AWACHANA BASATA NA DIAMOND, MSITAKE KUKWAMISHA SANAA YA BIASHARA
Tuesday, December 25, 2018
Msanii wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya Hip Hop, Wakazi ameweka wazi hisia zake kwa Diamond na Rayvann baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuwapunguzia adhabu wasanii hao kutoka lebel ya WCB kwa kuwaruhusu kufanya matamasha ya nje. Katika ukurasa wake wa Instagram Wakazi amewaomba Basata kuangalia namna bora ya kushirikiana na wasanii wote katika kuhakikisha wanafanya kazi zao vizuri na kuacha kukwamisha biashara ya muziki kwa kisingizio cha sera za utamaduni kwa mgongo wa Maadili na Desturi.
Aidha wakazi amemtaka Diamond kuacha kujitenga na wasanii wenzake kwa kutoshiriki vikao vya kujadili namna ya kuboresha mazingira ya sanaa nchini Tanzania kwani angeshiriki hapo awali katika mapambano ya kuishape Basata yasingemkuta yaliyomkuta.
Napenda kuwashukuru @basata.tanzania kwa kuwafungulia @diamondplatnumz & @rayvanny kufanya show zao za nje ya nchi. It was a wise decision, na imetuepusha from a lot of embarrassment. Ila kuna mambo ambayo ningependa kuyaweka wazi na ni muhimu to both parties involved in this debacle. MESSAGE TO BASATA: Lengo lenu kubwa ni kuidumisha sanaa na kutujengea wasanii mazingira ya kuifanya vyema. Dunia ya leo, Sanaa ni zaidi ya Utamaduni; ni Kazi, Burudani na pia Biashara kwa yule anayejihusisha nayo. Nawaomba msitumie sera za utamaduni kwa mgongo wa Maadili na Desturi, kuikwamisha Sanaa ya kibiashara, tena katika Jamii ambayo ina evolve kila kukicha. Baadhi ya misunderstanding zinazoendelea now, zisingekuwepo kama yale MAAZIMIO tuliyofanyia kikao (chini ya maagizo ya Waziri Mwakyembe) yangekuwa yameanza kutekelezwa. (Uhusishwaji, Rating System, etc). Let's not kill ART... being controversial & provoking is part and parcel of being artistic. A MESSAGE TO DIAMOND: We are all happy for your success (at least mimi binafsi I am). You are such an inspiration to many. You are powerful and have a lot of influence. Ila haujaitumia nafasi yako kuleta mabadiliko ya ukweli ya Sanaa, maana ulipohitajika kuongelea wanyonge hukufanya hivyo. Hadi ulitoa wimbo Wa "Mi Nakaa Kimya". Wakati wasanii wenzako tunapigana na BASATA na Wizara, wewe haukutupa support hata kidogo. Sisi as artists, ni "voices of the voiceless na Hopes for the hopeless". Ila indifference yako na lack of interest kwenye kui shape Basata, imechangia kufikia hadi leo sheria zinatishia kukuumiza wewe kimapato. Maybe ungekuwa unakuja kushiriki nasi tungekuwa tumei vunja BASATA na kuanzisha BASATA mpya inayoelewa kuwa the society is different, kuzingatia biashara, etc. Kuwa to mkaidi (Kwa Waziri Shonza, Basata) sio solution. Kwa nguvu uliyonayo ungeweza kusaidia sana ila inaonyesha we uliridhika as long as you were making money. Well "Karma is a B". Kuna Chama chetu cha TUMA (Tanzania Urban Music Association) hebu kuwa karibu, changia mawazo, onekana kwenye vikao. Utafanya kazi zako huru kabisa kama tutaibadilisha system, ila haitobadilika bila kujihusisha na kuungana na wenzako. Webiro "Wakazi" Wassira.
Social Plugin