Neema imewashukia wasanii nchini baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Hamisi Kigwangala kutoa ofa kwa wasanii wanaotaka kuandaa video za filamu ama za nyimbo zao katika maeneo ya utalii, kumuona yeye mwenyewe ili awape kibali cha kutumia vivutio hivyo vya utalii.
Kigwangala ameyasema hayo leo Desemba 15, 2018 katika uzinduzi wa chaneli ya Utalii iliyopewa jina la Tanzania Safari uliofanyika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam.
Dk Kigwangala amesema anafanya hivyo ili kukwepa urasimu mkubwa wanaopata wasanii wanapoomba kufanyia filamu ama video zao kwenye maeneo ya utalii nchini.
“Kila siku watanzania wanalalamika kuzuiwa kupiga picha katika baadhi ya maeneo na sasa hivi nimetoa ofa kwa wasanii wote wanaotaka kutengeneza video zao katika maene ya utalii wanione mimi moja kwa moja nitawapa vibali ili nawao watangaze vivutio vyetu,” amesema
Aidha amewatoa hofu watanzania wanaodhani Wizara ya yake haifanyi kazi ipasavyo wasiwe na wasiwasi kwani wamekuja na mkakati kabambe wenye lengo la kukuza sekta hiyo,
“Kwa sasa utalii unachangia asilimia 17.6 na tunasemwa sana kwasababu watanzania wanaona kama Wizara aifanyi kazi ipasavyo lakini nataka niwahakikishie kuwa tumejipanga na tuna mikakati mipya kabisa ya kuboresha sekta hii,” amesema
Social Plugin