Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAALIM SEIF KUHAMIA ACT WAZALENDO?



Chama cha Wananchi (CUF) upande wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba umedai Maalim Seif Sharif Hamad anajiandaa kuhamia ACT-Wazalendo.

Amesema Maalim Seif ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho kwa sasa yuko mbioni kutimkia ACT.

Akizungumza leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amedai vyama sita vya upinzani vilivyokutaka Zanzibar wiki iliyopita moja ya ajenda yao ilikuwa namna gani Maalim Seif atakubaliana na ACT-Wazalendo.

Amesema miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa upande wa Maalim Seif uachiwe nafasi zote za uongozi upande wa Zanzibar na Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa ACT, wachukue uongozi wa Tanzania Bara.

Amedai kuwa hata kama Maalim Seif ataondoka CUF, wataendelea kuwa imara huku akiwataka wote watakaoambatana na katibu mkuu huyo kwenda ACT kutosita kwa sababu uamuzi wao utaheshimiwa.

Mgogoro ndani ya CUF ulianza baada ya Lipumba kurejea katika uongozi mwaka 2016, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu alipojiuzulu. Jambo hilo liliibua mgogoro wa uongozi baada ya ofisi ya msajili kutangaza kumtambua Lipumba kama mwenyekiti na kusababisha pande hizo mbili kukimbilia mahakamani na kufungua kesi kadhaa ambazo zinaendelea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com