Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Diamond:WASAFI FESTIVAL NDIO SHOW NAMBA MOJA NCHINI, HUWEZI KUTAJA MUZIKI BILA WCB.


Rais wa WCB, Diamond Platnumz amedai show za Wasafi Festival ndio show namba mmoja nchini Tanzania kwa sasa kutokana na kuwakutanisha wasanii wakubwa kwa wakati mmoja

Platnumz amedai show nyingi ambazo zinafanyika bila wasanii wa WCB ni show za kawaida kutokana na kukosa wasanii wakubwa ambao wanatoka kwenye label hiyo kubwa ya muziki.

“Kusema kweli nategemea show zote za Wasafi Festival zijaze sana kwa sababu sisi hatujaonekana kwenye mikoa kwa muda mrefu, hatujawahi kuzunguka kwenye mikoa kwa muda mrefu. Halafu uzuri wa show zetu tunachanganyika wasanii wa WCB na wasanii wengine, lakini show nyingine sisi tunakuwa hatupo. Hii ina maana hizi ndio show namba moja nchini kwa sasa, ndio show ambazo zinawakutanisha wasanii wote, show nyingine huwezi kutaja muziki bila kutaja WCB,”

Chanzo; Bongo5

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com