Kikosi cha Yanga katika mchezo wa leo
Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tukuyu Stars katika uwanja wa taifa na kusonga mbele hatua ya 32 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Amissi Tambwe ambaye amefunga hat-trick katika dakika ya 14, 36 na 55 huku bao la mwisho likifungwa na Heritier Makambo katika dakika ya 88.
Pia mchezho huo ulikuwa ni wa kwanza kwa kiungo mpya wa klabu hiyo, Haruna Moshi 'Boban' aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili mwezi huu kutokea KMC.
Hata hivyo Boban hakuweza kumaliza mchezo, ambapo alitolewa dakika ya 28 ya kipindi cha kwanza kutokana na majeraha.
Yanga inasonga mbele hatua ya 32 bora ya michuano hiyo, ikiungana na kigogo Azam FC ambaye alicheza mchezo wake jana Desemba 23 na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Social Plugin