Kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mbeya City.
Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania klabu ya Yanga leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Kwa matokeo ya leo Yanga sasa inaendelea kuongoza ligi ikiwa na alama 50 ikifuatiwa na Azam FC wenye alama 40 baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 leo kutoka kwa Mtibwa Sugar.
Mshambuliaji wa Yanga mkongomani Heritier Makambo ndio alikuwa shujaa wa Yanga akifunga mabao yote mawili katika dakika za 11 na 41 kipindi cha kwanza wakati bao la Mbeya City likifungwa na Iddy Selemani.
Makambo sasa amefikisha mabao 11 kwenye ligi na kuongoza orodha ya wafungaji.
Yanga sasa imebaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi kuu msimu huu baada ya wenzao Azam FC kutibuliwa rekodi na Mtibwa Sugar huko Turiani Morogoro.
Wekundu wa msimbazi ambao wapo katika nafasi ya 3 wanashuka dimbani saa 1:00 kukipiga na Singida United kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam.
Via >>Eatv
Social Plugin