SOT, PRALENA KUCHANGISHA MILIONI 45

Taasisi ya Michezo ya watu wenye Ulemavu wa Akili Tanzania, Special Olympics inahitaji shilingi milioni 45 kwa ajili ya kuisaidia timu ya Taifa inayotarajia kushiriki michezo ya Dunia itakayofanyika mwezi Machi mwaka huu, Abu Dhabi Falme za Kiarabu (UAE).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays alisema fedha hizo ni kwa ajili ya tiketi za kwenda na kurudi sambamba na kambi ya maandalizi kuelekea katika michezo hiyo.

Rays alisema kambi ya maandalizi kwa siku 14 inahitaji shilingi milioni 10.5 huku tiketi kwa ajili ya kwenda na kurudi Abu Dhabi ni sh.milioni 34.5.

Aidha Rays alisema ili kufanikisha kushiriki katika michezo hiyo wameomba ridhaa ya Taasisi ya PRALENA Network Ltd ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa fedha hizo kupitia mfumo wa simu za mkononi.

Naye mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said alisema ili kufanikisha upatikaji wa fedha hizo wametengeneza mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha.

Said alisema mfumo huo utatumika kwa kila anayeguswa katika mitandao ya simu ya Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money.

“Tunawaomba wadau katika jamii, kusaidia kupatikana kwa fedha hizo kupitia Tigopesa, M-Pesa na Airtel Money kupitia namba ya kampuni 123123 na kumbukumbu namba ni 60024833555,” alisema Said.

Said aliweka bayana kauli mbiu ya ufanikishwaji wa fedha hizo ni ‘Ushindi wao ni ushindi wetu’.

Na Andrew Chale

Mwakilishi wa PRALENA, Thabit Said akizungumza namna ya mifumo mbalimbali ambayo wadau watachangia fedha ili kukusanya kiasi hicho cha Sh. Milioni 45.

Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuchangisha fedha za tiketi. Kulia ni Mwakilishi wa taasisi ya PRALENA, Bi. Irine Victor na kushoto ni Mjumbe wa bodi ya SOT, Makuburi Ally.

Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania (SOT), Charles Rays akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kuchangisha fedha za tiketi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post