Msanii wa muziki wa Hip Hop Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ameachia wimbo wake mpya unaoitwa “mafanikio” aliomshirikisha Barakah The Prince
Kupitia ukurasa wake wa instagram Fid Q amesema Amelazimika kutoa wimbo huo kutokana na ile kauli ya watu kudhani kuwa kufanikiwa ni kumiliki usafiri.
“Ile kauli ya mafanikio ni kumiliki gari ndio iliyopelekea mimi kuona umuhimu wa kuandika hii ngoma ili watu wetu wapate kujua maana halisi ya kufanikiwa ”, ameandika Fid Q
Social Plugin