Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania Dkt. Bashiru Ally amesema vyama vinavyotafuta wafuasi kwenye nyumba za ibada,mahakamani,mitandaoni safari yao siyo ndefu vitakufa kifo cha mende.
Dkt. Bashiru ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 7,2018 wakati akizungumza na wanachama wa CCM mkoa wa Shinyanga katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.
Amesema kutokana na vyama vya siasa kutafuta wafuasi kwenye misikiti,makanisa,mahakamani na mitandaoni haviwezi kufika mbali basi vitakufa kwa sababu ya kujitakia wao wenyewe.
Amesema kutokana na vyama vya siasa kutafuta wafuasi kwenye misikiti,makanisa,mahakamani na mitandaoni haviwezi kufika mbali basi vitakufa kwa sababu ya kujitakia wao wenyewe.
Ameviomba vyama vya siasa kutoshinda mahakamani kutafuta ruzuku na kwamba wanahitaji ushindani wa kweli wa maendeleo.
“Tunahitaji kujenga chama kwa misingi ya kidemokrasia,tunataka ushindani utawavutia watanzania kuendelea kutuamini,Kadri tutakavyojiimarisha tutakuwa chama mfano kwa vyama vingine
Aidha amewataka wanachama wa CCM kuacha tabia ya kutafuta ubunge na nafasi zingine za uongozi na badala yake wawaache viongozi waliochaguliwa watekelezea majukumu yao na muda utakapofika wa kufanya uchaguzi.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wanachama wa CCM katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga leo - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin