Baadhi ya wabunge na wageni waliofika bungeni hapo walionekana kumshangaa ndege huyo huku wakibaki na maswali namna alivyoingia kwenye ukimbi huo uliokuwa umefungwa.
Hata hivyo, hakuna aliyejua huyo bundi ameingiaje ndani ya ukumbi wa Bunge hasa kutokana na usalama na usafi ndani ya ukumbi huo.
Spika wa bunge, Job Ndugai, amemshuhudia Bunge huyo laivu na kusema alipomuona alichanganyikiwa kidogo na kisha akawatoa hofu Wabunge kuwa kwa Dodoma kumuona ndege huyo mchana si tatizo isipokuwa ukimuona usiku ndio unaweza kuogopa.
Watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge.
Ndege huyo hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Hata hivyo, haikujulikana muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.
"Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa," amesema Ndugai.
Social Plugin