Watu 200 hawajulikani waliko baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake katika mgodi wa kampuni ya chuma kusini mashariki mwa Brazil.
Maji yaliyochanganyika na matope yaliwafunika mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo.
Shughuli ya kuwatafuta manusura inaendelea karibu na mji wa Brumadinho, katika jimbo la Minas Gerais.
Gavana wa jimbo hilo Romeu Zema amesema kuna hofu huenda watu wengi wamefariki katika mkasa huo.
Kufikia sasa watu tisa wamethibitishwa kufariki.Barabara zilizoharibiwa zinatatiza oparesheni ya kuwatafuta manusura
Baadhi ya watu waliyokwama kwenye matope, waliokolewa kwa kutumia helikopta baada ya barabara kuharibiwa.
Watu wengine wamehamishiwa kutoka makaazi yao kutokana na sababu za kiusalama.
Kwa mujibu wa afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya Vale, Fabio Schvartsman thuluthi moja ya wafanyikazi karibu 300 hawajulikani waliko.
"Nina hofu nataka kujua hali ni mbaya kiasi gani'' alisema Helton Pereira mmoja wa jamaa za watu waliyoathiriwa na mkasa huo aliyezungumza na BBC nje ya hospitali ya Belo Horizonte.
Anasema mke wake na dada yake wote hawajulikani waliko kwa sababu walikuwa wanaendesha biashara ya chakula karibu na eneo la tukio.
Shughuli ya kuwatafuta manusura inafanywa na maafisa 100 wa kukabiliana na hali ya dharura huku wengine zaidi wakitarajiwa kupelekwa katika eneo hilo.
"kuanzia sasa matumaini ya kuwapata waliyohai havuna pengine tutoe miili iliyokwama kwenye matope," alisema gavana Romeu Zema wa jimbo la Minas Gerais.Bwawa hilo linamilikiwa na kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Vale, Brazil
Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ametaja mkasa huo kama ''janga la kitaifa''.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika "Tunajaribu kila tuwezalo kuwaokoa manusura zaidi wa mkasa huu,".
Maafisa wengine wakuu serikalini wamezuru eneo hilo.Watu wengi wanahofiwa kufariki baada ya bwawa la maji kuvunja kingo zake kusini mashariki mwa Brazil.Maji yaliyochanganyikana na matope yalisomba mkahawa wa chakula uliyokuwa na mamia ya wafanyakaziRais Jair Bolsonaro pamoja na maafisa wengine wakuu serikalini wanatarajiwa kuzuru eneo la mkasa
Social Plugin