Chura anayeaminika kuwa wa mwisho wa aina yake katika ulimwengu ameondolewa upweke.
Romeo, anayejulikana kama chura wa pekee ulimwenguni, ameishi miaka 10 ya kutengwa katika hifadhi ya Bolivia.
Wanasayansi wanasema wamempatia mchumba kwa jina Juliet baada ya safari ya kwenda msitu wa Bolivia.
Chura watano wa majini walipatikana katika vidimbwi vya maji na kukamatwa, kwa kusudi la kuzalishana na kupandikiza upya wanyama hao kwenye pori.
Teresa Camacho Badani ni mkuu wa kitengo cha viumbe hai katika hifadhi asili iliyopo Cochabamba na kiongozi wa safari hiyo.
Anatarajia kwamba vyura hao wa jinsia tofauti watapaendana: "Romeo ni mtulivu na hana mizunguko," aliiambia BBC. "Romeo ana afya na anapenda kula, lakini ana aibu na mpole."
Chanzo:Bbc
Social Plugin