Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DAWASA YAKABIDHIWA JENGO, WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa DAWASA kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa machache.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya wajenzi wa kampuni ya CCECC ambao ndiyo wakandarasi. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni kulia ni mmoja ya mkandarasi msahauri wa jengo hilo. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) akimkabidhi makataba wa kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020. Pambeni anayeshuhudia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto).
Wafanyakazi wa DAWASA na wageni waalikwa wakifuatiliwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage (anayefuata kushoto) wakifurahi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) mara baada ya kuzindua picha ya jengo la Maji linalotarajiwa kumalizika Februari 2020.
Muonekano wa jengo la Maji litakalohamishiwa ofisi za DAWASA mara baada ya kumalizika.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa.

Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama.

Mkumbo amesema hayo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya jengo la Maji lililopo Ubungo jijini Dar es Salaama na linalotarajiwa kumalizaika Februari 2020.

Utiaji wa saini hiyo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Akizungumza baada ya utiaji wa saini, Mkumbo amesema DAWASA lazima wahakikishe wanasimamia mapato ili kuweza kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kufaidika.

Amesema, hafla ya leo sio ya kukabidhiwa jengo tu ila wanatakiwa kusimamia mradi wa Kidunda, visima vya Kimbiji Mpera pamoja na kuwaunganishia wateja wapya.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Mwamunyage amesema changamoto kubwa iliyokuwepo katika mamlaka hiyo ni maeneo ya kufanyia kazi ila baada ya kukabidhiwa jengo hilo wanaamini kwa sasa kazi zitafanyika kwa wakati.

Amesema, kwa sasa DAWASA wanajiendesha wenyewe kwa mapato ya ndani na watasimamia mpaka kumalizika Februari 2020.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Luhemeja amewashukuru Wizara kwa kuwakabidhi jengo hilo lenye ghorofa 15 kwa ajili ya kuweka ofisi na itawasadia kufanya kazi kwa uharaka zaidi na ameahidi kuwa jengo hilo litakamilika kwa wakati kwani tayari ameshamuagiza Mkurugenzi wa Fedha kuanza kufanya malipo.

Pia ameeleza kuwa kwa sasa DAWASA ndani ya miezi mitatu wameweza kufikia malengo ya kufikia Bilioni 10 kwa mwezi katika ukusanyaji wa maji ila wamejizatiti kwa mwaka huu kufikia malengo ya serikali ya upatikanaji wa maji mijini na vijijini kabla ya 2020 ikiwemo na kupunguza mivujo kwa asilimia 25.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com