Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga imeanzisha dawati maalumu litakalosikiliza na kushughulikia vitendo vya rushwa ya ngono kwa wanafunzi wa shule na vyuo ambao wametajwa kukabiliwa na kadhia hiyo kwa muda mrefu.
Kaimu mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Francis Luena alibainisha hayo jana Jumatatu 21,2019 wakati akitoa taarifa ya utendajikazi wa taasisi hiyo kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba 2018 kwa waandishi wa habari.
Alisema kuanzishwa kwa dawati hilo ni miongoni mwa mikakati itayotoa fursa kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa sehemu sahihi ya kukimbilia kutoa taarifa wakati wanapokutana na mkasa huo.
Alisema kuanzishwa kwa dawati hilo ni miongoni mwa mikakati itayotoa fursa kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa sehemu sahihi ya kukimbilia kutoa taarifa wakati wanapokutana na mkasa huo.
“Tuliwahi kufanya utafiti wa rushwa ya ngono kwenye shule za msingi,kwa kweli ule utafiti ulisikitisha tulibaini baadhi ya walimu wanatumia mbinu ya kumchapa viboko na kumpatia adhabu kali mwanafunzi kumbe lengo lake ni kumtaka mwanafunzi huyo kingono,kwa hiyo dawati hili litatoa mwanya kwa wanafunzi kuleta taarifa hizo na kuweza kufanyiwa kazi,” alisema Luena.
Wakizungumza na www.malunde.com, baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Mtakatifu Joseph mkoani Shinyanga wamekiri kuwepo kwa vitendo vya manyanyaso ya kingono kutoka kwa wakufunzi katika baadhi ya vyuo
na kueleza kuwa hatua ya kuanzishwa kwa dawati hilo itasaidia kupunguza vitendo vya rushwa ya ngono vinavyowaathiri wanafunzi kisaikolojia.
na kueleza kuwa hatua ya kuanzishwa kwa dawati hilo itasaidia kupunguza vitendo vya rushwa ya ngono vinavyowaathiri wanafunzi kisaikolojia.
Kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na.11 ya mwaka 2007 imeitaka taasisi hiyo kuchunguza,kuelimisha umma na kufanya utafiti , kwenye miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wanaojihusisha na masuala ya rushwa.
Na Malaki Philipo - Malunde1 blog
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡