Facebook ina mipango ya kuunganisha huduma zake za kutuma ujumbe katika Instagram, WhatsApp na Facebook Messenger.
Licha ya kwamba huduma zote tatu zitasalia kuwa programu huru zitashirikiana kupitia ujumbe utakaotumwa kutoka huduma moja hadi nyingine.
Facebook imeambia BBC kwamba ndiyo mwanzo wa mchakato mrefu.
Mpango huo kwanza uliripotiwa mjini New York na unaaminika kuwa mradi wa kibinafsi wa mwanzilishi wa facebook Mark Zuckerberg.
Utakapokamilika , ushirikiano huo utamaanisha kwamba mtumiaji wa facebook anaweza kuwasiliana moja kwa moja na mtu ambaye anamiliki akaunti ya WhatsApp.
Hili haliwezekani kwa sasa kwa kuwa programu zilizopo hazina uhusiano.
Hatua ya kuunganisha huduma hizo tatu umeanza , kulingana na gazeti la The new York Times na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019 ama mapema mwaka ujao.
Je facebook ina mpango gani?
Facebook haikupendelea kuzungumzia kuhusu swala hili katikati mwa kashfa ilioikumba, lakini ililazimishwa na watu waliokuwa wakiwasiliana na New York Times.
Hadi kufikia sasa , WhatsApp, Instagram na Messenger zimekuwa zikifanya kazi kivyake na kushindana kibiashara.
Kuunganisha huduma hizo kwaa kutuma ujumbe kutarahisisha kazi ya facebook.
Haitalazimika kuunda programu mpya kama vile stories ambapo huduma zote tatu zimeongeza katika programu yake bila mafanikio ya kufurahisha.WhatsApp, Messenger na Instagram ni bidhaa huru zinazoshindana
Mawasiliano ya ujumbe kupitia huduma moja hadi nyengine yanaweza kuimarisha biashara katika huduma moja kwa kutuma ujumbe kwa huduma nyengine.
Pia yatairahisishia facebook kugawana data katika huduma zote tatu ili kusaidia juhudi za matangazo yake.
Hatua hiyo pia itaimarisha uwepo wa facebook na kuwa vigumu kuanguka iwapo serikali husika zitajaribu kuivunja kwa manufaa yao ya kibinafsi.
Usambazaji wa data.
Bwana Zuckerberg ameripotiwa kushinikiza ushirikiano huo ili kuimarisha huduma za kampuni yake kuwa muhimu na kuongeza muda wa wakati unaotumika na wateja wake katika huduma hizo.
Kupitia kuunganisha wateja wake katika kundi moja kubwa, facebook itaweza kushindani vizuri na kampuni ya Google na Apple iMessage kulingana na Makena Kelly wa mtandoa wa habari wa The Verge.
"Tunataka kuunda huduma bora zadi ya kutuma ujumbe ilio na ulinzi wa hali ya juu na kufanya kuwa rahisi kuwafikia marafiki na familia kupitia huduma tofauti'', aliongezea.
Taarifa hiyo ilisema kuwa kulikuwa na majadiliano na mjadala kuhusu vile mfumo huo utakavyofanya kazi.
Kuunganishwa kwa huduma hizo tatu kuteleta mabadiliko muhimu katika kampuni ya facebook kwa kuwa imeruhusu Instagram na WhatsApp kufanya kazi kama kampuni tofauti zilizo huru.
Gazeti la the New York Times linasema kuwa hatua ya Bwana Zuckerberg kupigania mpango huo wa kuunganisha huduma hizo umesababisha mgogoro wa ndani.
Inadaiwa ndio sababu ya waanzilishi wenza wa Instagram na WhatsApp kuondoka mwaka uliopita.
Hatua jhiyo inajiri huku facebook ikikabiliwa na uchunguzi na kukosolewa kuhusu vile inavyotunza data za wateja wake.
Chanzo - BBC