Leo Januari 23, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na viongozi mbalimbali wa Dini Ikulu Dar es Salaam na kuongea nao.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima alipata nafasi ya kusimama na kuongea mbele ya Rais Magufuli.
“Mchungaji Lyimo ameshauri ziwekwe sheria ili madhehebu yapungue, mimi nina mawazo tofauti na yeye, ukiangalia baa zipo nyingi hadi wengine wananywea chini ya mti, na pombe imesemwa kwenye vitabu vya dini siyo nzuri kwetu sote, Wakristo na Waislam.
“Pale Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar kuna msikiti kwa ajili ya Waislam, nilikuwa naomba pia kujengwe pia Kanisa kwa ajili ya Wakristo kuabudu ili kuleta usawa. Suala la kuabudu ni muhimu sana katika mazingira ya kazi.
“Nakupongeza sana, umefanya jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia, tumekuja kwa pamoja na kwa upendo kujadili mambo ya mbalimbali ya nchi Mungu atakusaidia sana na kukuinua sana katika utawala wako” , amesema Askofu Josephat Gwajima.
Social Plugin