Jeshi la Polisi limetangaza mabadiliko ya Makamanda wa Mikoa mitatu ikiwemo Ng'anzi (Arusha), Hamduni (Ilala) na Lukula (Temeke) ambapo wamehamishiwa makao makuu ya polisi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola.
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Nchini ambayo ilimnukuu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ahmed Msangi, Makanda hao watatu wamerudishwa makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa madai yao.
Hatua ya kuchungunzwa kwa Makamanda wa mikoa hiyo ni kufuatia maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola alilolitoa wiki iliyopita kwamba walishindwa kutekeleza baadhi ya maagizo ambayo walipewa na wizara.
Mapema wiki iliyopita Lugola alisema hadhani kwamba maagizo hayakupuuzwa bali yangeweza kutekelezwa muda wowote.
Kangi Lugola alisema "sina taarifa kwamba agizo langu halijatekelezwa lakini kwa sababu nilimpa muda wa utekelezaji IGP kwa hiyo naamini litatekelezwa, saa nyingine watu hawajui kutengua mtu ni mamlaka na mimi ndiye nina mamlaka."
"Utekelezaji ndiyo unaendelea sidhani kama wamekaidi au IGP amekaidi kutekeleza agizo langu." aliongeza Kangi Lugola.
Social Plugin