Mwanaume mwenye umri wa makamo kutoka Maralal kaunti ya Samburu amefungwa jela kwa siku 30 baada ya mahakama kumpata na hatia ya kutumia lugha chafu kwa aliyekuwa mpenzi wake.
Mshukiwa Joseph Naroto anasemekana kumtusi mpenzi wake wa zamani Winnie Letito kuwa yeye ni kahaba na mwanamke mzee.
Naroto anasemekana kukopa pesa kutoka kwa Winnie wakati wakichumbiana ila alipotaka arejeshe pesa hizo mwezi Septemba mwaka wa 2017, mshukiwa alianza kuwa mkali na kumrushia cheche za matusi kila mara.
Kesi dhidi ya Naroto ilisikizwa Jumanne, Januari 29 ambapo alikana mashtaka hayo na mahakama iliamru mshukiwa azuiliwe kwa siku 30 baada ya kushindwa kulipa dhamana ya KSh 3,000.
Chanzo:Tuko
Social Plugin