Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amedai Tanzania ya zamani ilikuwa ikiishi kama nchi yenye laana kutokana na baadhi ya rasilimali zake kutumika zaidi na wageni na kushindwa kuwafaidisha watanzania wenyewe.
Askofu Kakobe ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa wadau wa uchimbaji na wafanyabiashara ambapo walizungumza na Rais John Pombe Mgufuli ili kuhakikisha sekta hiyo inainua uchumi wa Tanzania.
“lakini ni jambo la kushukuru kwa sababu Mungu amemuinua shujaa Rais Magufuli ambaye amekataa kwamba tuachiwe mashimo na urithi wetu wachukue mataifa mengine na suala hili linahitaji ushujaa sana,” Askofu Kakobe alisema,.
“hata Biblia inasema tutangulize yaliyo mema hata kama una hasira naye, hata Yesu Kristo alipokuwa anatoa ujumbe kwa makanisa saba alikuwa anaanza kupongeza mazuri hata kabla ya kuinua jambo lolote la kupinga, atakayekuwa anapinga atakuwa ni mkorofi na hata ukiwa na hoja itakuwa ngumu kusikilizwa,” ameongeza Askofu Kakobe.
“Mimi nafikiri unapoanza kupambana na suala hili, uanze kufanyia kazi kwanza fikira za mtu. Kadiri tunapozidi kutamka vitu vizuri ndiyo tunazidi kuvichochea,” aliongeza Kakobe.
Chanzo:Eatv
Social Plugin