Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe amesema hajawahi kumiliki kadi ya chama chochote cha siasa nchini, bali amekuwa akishiriki shughuli za vyama hivyo kutokana kupewa mialiko kufika kama mtumishi wa kiroho.
Kakobe ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa muendelezo wa ibada yake ya kila Jumapili kanisani kwake ambapo hana mahusiano na viongozi wowote wa kisiasa hasa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Kakobe amesema, "sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha Chadema wala CCM, na sina kadi ya vyama hivyo, na wala sijawahi kuwasiliana na kiongozi yoyote wa CHADEMA wala kuonana nao ana kwa ana, wala hawajawahi kuja ofisini kwangu, halijawahi kutokea"
Aidha ameongeza kuwa, "niliwahi kuitikia mwaliko wa chama cha CHADEMA mara moja tu miaka michache iliyopita kwenye mkutano uliofanyika eneo la Mlimani City na nilienda kama baba anayeweza kualikwa na watoto".
Kiongozi huyo amesema hayuko tayari kupokea nafasi yeyote kama akiteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile alichokidai kuwa tayari anayo kazi ya kufanya ambayo ni kumtumikia Mungu.
"Hata Rais Magufuli akiniteua Leo siwezi kukubali, nitamueleza nina kazi maalum ya kumtumikia Mungu, siwezi kuwa mbunge alafu nikakaa bungeni miezi mitatu niache kumtumia Mungu".
Chanzo - EATV
Social Plugin