Wabunge wa Uingereza Jumanne waliyakataa pakubwa makubaliano ya Waziri Mkuu Theresa May na Umoja wa Ulaya kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja huo, jambo lililouvuruga mchakato wa Brexit.
Hatua hiyo imepelekea kura isiyokuwa na imani kuwasilishwa, hatua ambayo inaweza kuiangusha serikali ya May. Wabunge walioyapinga makubaliano hayo ni 432 huku walioyaunga mkono wakiwa 202 pekee.
Kushindwa kwa Waziri Mkuu huyo kulitarajiwa na wengi ingawa kiasi cha kura alizoshindwa nazo ni jambo ambalo limeuharibu uongozi wake unaosuwasuwa.
Kushindwa huku ni kwa kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa serikali kushindwa kwa kiasi kikubwa cha kura katika bunge la Uingereza na kunafuatia msukosuko wa kisiasa wa zaidi ya miaka miwili ambapo May alijiwekea hadhi ya kisiasa kwa kuhakikisha amepata makubaliano ya Brexit.
Jeremy Corbyn aliwasilisha mswada wa kutokuwa na imani na serikali ya May
Muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa na spika John Bercow Waziri Mkuu May, alizungumza.
Chanzo:Dw
Social Plugin