Marekani na China wanaanza duru tete ya mazungumzo kuhusu biashara huku kukiwa na matumaini finyu ya kufanikiwa kutokana na masharti ya viongozi wa mjini Washington kulazimisha mageuzi katika mfumo wa kiuchumi wa China.
Pande hizo mbili zitakutana si mbali na ikulu ya Marekani kwa mazungumzo ya ngazi ya juu kabisa kuitishwa tangu rais Donald Trump na rais wa China Xi Jinping walipokubaliana Desemba iliyopita, kipindi cha siku 90 cha utulivu katika vita vyao vya biashara.
Kwa miezi kadhaa sasa mvutano wa kibiashara umekuwa ukiendekea huku kukiwa na maoni tofauti yanayotolewa na rais Trump kupitia mtandao wa Twitter, mara yakiwa ya kutia moyo na mara nyengine ya vitisho.
Wiki iliyopita tu Rais Trump alisema ameridhika na jinsi mazungumzo yalivyoendelea hadi sasa. Amesema ana hakika "China inapendelea sana kufikia maridhiano.
Matamshi kinyume na hayo lakini yalitolewa na waziri wake wa biashara Wilbur Ross ambae hatarajii makubaliano yoyote kufikiwa katika mvutano wa biashara pamoja na China.
Chanzo:Dw
Social Plugin