Mungu, bidii, kujituma kwa walimu pamoja na wanafunzi zimetajwa kuwa sababu za ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa shule ya sekondari St. Francis iliyopo mkoani Mbeya.
Shule hiyo ya wasichana imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne iliyofanyika mwaka jana ikiwa na ufaulu wa daraja la kwanza kwa wanafunzi wote.
Akizungumza na MCL Digital leo kwa niaba ya mkuu wa shule hiyo mwalimu wa nidhamu, Neema Kimani amesema Mungu kuwa wa kwanza na kujituma kwa walimu na wanafunzi, imekuwa chachu ya mafanikio hayo makubwa
"Tumekuwa tukimtanguliza Mungu kila wakati na kuwalea kama watoto hivyo wanakuwa huru kwetu na kueleza shida zao," amesema Neema.
Leonard Peter mmoja wa walimu katika shule hiyo amesema nafasi hiyo ni muhimu na ina maana kubwa kwani matokeo ya mwaka huu ni bora kuliko miaka ya nyuma.
Atia Mwasongwe, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo, amesema matokeo hayo yanawapa nguvu na kuona hakuna kitu kinachoweza kuzuia wao pia kufanya vizuri.
Na Yonathan Kossam, mwananchi.
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2018 NA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2018 YAMETANGAZWA.YAANGALIE HAPA CHINI KWA KUBONYEZA LINK
Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
Kuwa Mjanja..Download App mpya ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Social Plugin