Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AUAWA KWA KUKATWA PANGA NA MUMEWE KISA ADA YA SHULE


MAUAJI – KYELA.
Mnamo tarehe 21.01.2019 majira ya saa 00:15 usiku wa kuamkia leo huko Hospitali ya Wilaya ya Kyela, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya. HAWA KAMWELA [27]  mkazi wa kijiji cha Busale,  Kata ya Busale, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela na Mkoa wa Mbeya alifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kukatwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na mume wake  aitwaye ZAWADI KYEJO, mkazi wa Kijiji hicho cha Busale.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya wanandoa hao baada ya mtuhumiwa huyo kukataa kutoa ada ya shule ya mtoto wao aitwaye SYLIVESTER ZAWADI aliyefaulu mtihani wa darasa la saba mwaka 2018.  Mbinu iliyotumika ni kumvizia marehemu huyo akiwa amelala na kumshambulia kwa panga. Msako mkali wa kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa huyo  ili kumfikisha katika vyombo vya sheria unaendelea.

MAUAJI – KYELA.
Mnamo tarehe 19.01.2019 majira ya saa 11:03 asubuhi huko kituo cha afya Ipinda, Kata ya Ipinda , Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. MUSSA KATINA [35], mkazi wa Kijiji cha Mwaigoga alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kwenye kituo hicho cha afya kutokana na kukatwa katwa na panga kichwani na sehemu nyingine za mwili wake na LWITIKO MWAKAROBO [50] mkazi wa Ipanda, Tarafa ya Ntebela.

Marehemu huyo ni mdogo wa mtuhumiwa huyo wakiwa ni ndugu waliozaliwa na mama na baba mmoja. Kiini cha tukio hilo bado hakijafahamika mpaka sasa. Mbinu iliyotumika ni kumvizia marehemu huyo na kumshambulia ghafla kwa kumkata panga kichwani, Mwili wa marehemu  umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya Wilaya Kyela ukisubiri uchunguzi wa kitabibu. Mtuhumiwa amekamatwa. Upelelezi unaendelea.
KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KULIPIA USHURU.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili [02] 1. LEAH MWAKAJILA [42] Mkazi wa Uyole na REHEMA MATOLA [42] Mkazi wa Kiwira wakiwa na vitenge doti 72 toka nchini malawi wakiviingiza nchini bila kulipia ushuru.

Watuhumiwa walikamatwa tarehe 21.01.2019 saa 14:30 mchana huko katika Road Block Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani.

KUINGIZA VIFARANGA NCHINI VILIVYOPIGWA MARUFUKU.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tukuyu iliyopo Wilaya ya Rungwe aitwaye MICHAEL PASCHAL [50] mkazi wa msasani akiwa na vifaranga box 04 sawa na vifaranga 400 toka nchini malawi vilivyopigwa marufuku kuingizwa nchini .

Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 19.01.2019 saa 15:00 alasiri huko katika road block Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya akiwa na vifaranga hivyo, akiviingiza nchini kinyume cha sheria. Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com