Timu ya Kariobangi Sharks imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
Sasa kwa mara nyingine fainali ya SportPesa Super Cup nchini Tanzania itazikutanisha timu za Kenya baada ya wenyeji kuondolewa mapema kama ilivyokuwa mwaka 2017.
Na hizo ni Kariobangi Sharks na Bandari FC ya Mombasa ambayo yenyewe imetinga fainali kwa kuwatoa vigogo wa Tanzania, Simba SC leo kwa kuwachapa mabao 2-1.
Mwaka jana nchini Kenya, wenyeji Gor Mahia wakitwaa taji hilo kwa mara ya pili walikutana na Simba SC ya Tanzania na kuibuka na ushindi wa 2-1 katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
Lakini Gor Mahia msimu huu walitupwa nje mapema tu na Mbao FC kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 kwenye mechi za Robo Fainali.
Social Plugin