Makachero kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) wamemkamata afisa wa zamani wa kikosi cha jeshi la Ulinzi Kenya (KDF) aliyekuwa akijidai kuwa afisa wa Ujasusi wa Jeshi la Ulinzi (DMI) Kaunti ya Lamu.
Hassan Ali Wario, 36, alikamatwa Jumamosi Januari 19, wakati alipoingia katika Kituo cha Polisi cha Kiunga, Lamu Mashariki na kujitambulisha kuwa afisa wa Ujasusi wa Jeshi la Ulinzi.
Ripoti ya polisi imesema Wario alikuwa akifanyia kazi yake katika kambi ya wanajeshi wa majini eneo la Kiunga Masura.
“Baada ya kumhoji tuligundua alikuwa afisa wa zamani wa KDF na alijiuzulu Januari, 2018,"
Bwana huyo wa jamii ya Waborana sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu, Januari 21, 2019 ingawa haijabainika lengo lake lilikuwa nini hasa kipindi hiki polisi nchini Kenya wanatafuta chanzo cha shambulio la kigaidi la Jumanne, Januari 15, lililotokea katika hote dusitD2 katika eneo la 14 Riverside Drive, Nairobi.
Wiki kadhaa zilizopita, maafisa wa KDF waliokuwa wakikuruta wanajeshi wapya, waliwakamata vijana kadhaa wakiwa na barua feki za mwaliko kujiunga na kambi ya mazoezi.
Visa vya watu kujifanya maafisa wa jeshi la KDF vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara na itakumbukwa katika miaka ya nyuma, Joshua Waiganjo alikamatwa baada ya kufanya kazi miaka mingi akijifanya kuwa afisa wa polisi.
Social Plugin