Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANDISHI WA HABARI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Mwandishi wa habari za upelelezi nchini Ghana amepigwa risasi hadi kufa wakati akiendesha gari kwenda nyumbani, baada ya mwanasiasa kuitisha adhabu dhidi yake.


Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa watu wasiojulikana wakiwa katika pikipiki walimpiga risasi Ahmed Hussein-Suale mara tatu katika mji mkuu wa Accra.

Alikuwa ni miongoni mwa wahusika wa shirika binafsi la upelelezi Tiger Eye na alipepeleza rushwa katika ligi ya mpira wa miguu Ghana.


Taarifa hiyo ya uchunguzi kuhusu rushwa ilisababisha kufungiwa maisha kwa aliyekuwa kiongozi wa shirikisho la kandanda nchini Ghana.

BBC Afrikan Eye ilifanya makala kuhusu skendo hiyo mwaka 2018 baada ya kupata uchunguzi huo kwa ruhusa ya mwandishi machachari Anas Aremayaw Anas, ambaye anaiongoza Tiger Eye.

Baada ya BBC kurusha makala hiyo, mbunge wa Ghana Kennedy Agyapong alisambaza picha za mwandishi huyo Hussein-Suale na kutaka adhabu dhidi yake.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com