Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKE AMCHOMA MMEWE KWA MAJI YA MOTO SEHEMU ZA SIRI

Jamaa mmoja mwenye umri wa makamo amekimbizwa hospitalini kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya baada ya mkewe kumchoma kwa maji moto kwenye sehemu nyeti/sehemu za siri. 

Inaelezwa kuwa jamaa huyo alipigiwa simu na mmoja wa wateja wake wa kike akimjuza kuhusu nafasi ya kazi ila mkewe alidhani alikuwa akizungumza na mchepuko wake.
 
Mwanamke aliingia hadi jikoni akiwa amejawa na hasira, akachemsha maji na kisha akamumwagia mumewe kwenye sehemu zake za siri na mgongoni.

 "Nilipigiwa simu na mmoja wa wateja wangu wa kike akinieleza kuhusu nafasi ya kazi lakini mke wangu alijawa na ghadhabu na kuanza kunikashifu kwa kutokuwa mwaminifu katika ndoa," Mwathiriwa alisema. 

 "Mke wangu alienda jikoni, akachemsha maji na muda mfupi baadaye alirudi na maji moto kwenye sufuria na kunimwagilia kwenye sehemu nyeti na mgongoni," Jamaa huyo aliongezea.

 Aidha, jamaa huyo ambaye anapokea matibabu katika hospitali ya Kimbimbi alisema mkewe wa miaka 12 katika ndoa amekuwa akitishia mara kadhaa kumchoma. 

Via Tuko blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com