Dakika 90 za mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya JS Saoura katika Uwanja wa Taifa zimemalizika wa Simba kuichapa JS Saoura mabao 3 -0.
Dakika ya 45 Okwi alifanikiwa kutumia uwezo wake wa mguu wa kushoto kumalizia pasi ya Clyetous Chama ambaye alipiga pasi mpenyezo iliyomkuta Okwi akawaminya mabeki waarabu na kumalizia kwa shuti kali.
Dakika ya 52 Okwi anamtengenezea pasi Kagere ambaye anaandika bao la pili kwa Simba.
Dakika ya 63 Kagere akamalizia pasi ya Okwi na kuandika bao la tatu kwa Simba Uwanja wa Taifa
SOMA ZAIDI HAPA
Social Plugin