Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAULI YA PAPA FRANCIS KUHUSU MAPADRI KURUHUSIWA KUOA

Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesema suala la kutooa kwa mapadri ni “zawadi kwa Kanisa” na si hiari, akiondoa matumaini kwa viongozi hao wa kidini kuoa.


"Binafsi nadhani suala la ukapera ni zawadi kwa Kanisa," Papa aliwaambia waandishi wa habari leo Jumatatu Januari 28) wakati akiwa kwenye ndege akirejea Vatican kutoka Panama alikohudhuria Siku ya Vijana Duniani.

"Pili, sidhani kama suala la hiari katika ukapera linatakiwa liruhusiwe. Hapana," alisema.

Papa hata hivyo alikiri kuwa “kuna uwezekano kwa sehemu zilizo mbali kufikika ", kama visiwa vya Pasific au Amazon ambako alisema "kuna umuhimu wa huduma za kipadri ".

"Hili ni suala linalojadiliwa na wanathiolojia, si uamuzi wangu," alisema.

Papa huyo raia wa Argentin amekuwa akisema kila mara kuwa hakuna zuio la kudumu kwa watu waliooa kuwa mapadri na hivyo suala hilo linaweza kubadilishwa.

Saint Peter (Mtakatifu Petro), kanisa la kwanza la papa, lilikuwa na mama mkwe, kwa mujibu wa Biblia.

Ukapera uliingizwa karne ya kumi na moja, inawezekana baadhi ya sababu zilikuwa ni kuzuia uzao wa mapadri kurithi mali za kanisa.

Baadhi, ndani ya Kanisa, wanaamini wakati umefika wa kuungana na makanisa mengi ya Katoliki ya mashariki kuruhusu wanaume waliooa kuvaa majoho ya upadri. Mapadri walioa wa Kanisa la Anglikana ambao wanataka kujiunga na Kanisa Katoliki, wameshakaribishwa.

Kiongozi wa pili kwa mamlaka wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, aliwahi kusema katika mahojiano mwaka jana kuwa kanisa “kidogokidogo litaangalia suala hilo kwa mapana" lakini akasema hakutakuwa na mabadiliko ya haraka.

 AFP

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com