Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NGULI WA SOKA MAKELELE : PAUL POGBA ANA DHARAU WAPINZANI


Wachezaji wakongwe mbalimbali (kwenye duala jeusi ni Claude Makélélé.

Kiungo wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Claude Makelele amesema mtindo wa ushangiliaji mabao wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba ni kutoheshimu wapinzani wake.

Makelele ameeleza kuwa Pogba hastahili kufanya hivyo mbele ya wapinzani wake kwani sio jambo la busara kimichezo.

"Kumfunga mpinzani wako goli 4 kisha unacheza mbele yake baada ya mchezo sio jambo la hekima kwa mpinzani hata kidogo. Huko ni kudharau wapinzani wake aliowafunga", ameeleza Makelele.

Makelele amesisitiza kuwa kila mchezaji huwa anafurahi anapopata ushindi au kufunga bao lakini mambo kama hayo ayafanye kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Tangu kuondoka kwa Jose Mourinho na kuteuliwa kwa Ole Gunnar Solskjær Pogba amekuwa kwenye wakati mzuri akifunga mabao 4 na kusaidia matatu kwenye mechi 3 walizocheza mpaka sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com