Mary Wambui akiwa na mmewe Joseph Kori
Joseph Kori akiwa na mchepuko wake (Judy Wangui)
Wakazi wa mtaa wa Juja katika Kaunti ya Kiambu wamejawa na huzuni baada ya jamaa mmoja kumuua mke wake kisha kutupwa mwili wake katika bwawa la maji siku ya Jumamosi, Januari 26, kufuatia kashfa ya kimapenzi.
Mary Wambui anadaiwa kuuawa na mume wake Joseph Kori kwa ushirikiano na mwanamke mwingine (mchepuko) Judy Wangui.
Joseph Kori Karue na mchepuko wake Judy Wangui Mungai sasa wanazuiliwa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya Mary Wambui Kamangara.
Wangui alikuwa mfanyakazi wa zamani wa Kamangara na kulingana na ripoti zilizosambaa ni kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wa bosi wake.
Kori alikamatwa eneo la tukio na awali alikuwa ameripoti polisi kuhusu kutoweka kwa mke wake na hata kuwapeleka polisi katika nyumba ya Wangui ambapo matone ya damu yalipatikana.
Mwanamke huyo aliyedaiwa kushrikiana na mpenziwe wa Kiambu kumuua mkewe alichukua nafasi ya kuchapisha facebook picha walizopiga pamoja licha ya kujua kuwa huyo alikuwa mume wa mtu.
Inaelezwa kuwa Wangui alitumia ukurasa mbadala kwenye Facebook kuzichapisha picha kadhaa akiwa na mume huyo wakiponda raha.
Inadaiwa kuwa Kamangara alijeruhiwa vibaya baada ya kutokea ugomvi nyumbani kwake na Wangui Jumamosi, Januari 26.
Mapema siku hiyo, Wangui aliabiri/alikodi taxi kwenda kumuona Kori nyumbani kwao alikokutana na Kamangara aliyekuwa bosi wake wa zamani.
Judy Wangui (pichani) anadaiwa kuanza uhusiano wa kimapenzi na Kori miaka miwili iliyopita na inaelezwa aliishi maisha kifahari na inadaiwa kuwa maisha yake yalibadilika kabisa baada ya kuanza uhusiano na Kori.
Maafisa wa polisi walipata alama za damu kwenye nguo zake baada ya mwili wake kupatikana karibu na bwawa moja eneo hilo.
Kwa mujibu wa Daily Nation, Wangui alikuwa mkazi wa Thindigua, kaunti ya Kiambu na alikuwa akiuza nguo za mitumba.
Social Plugin