Afisa mmoja wa polisi Kaunti ya Kisumu ametiwa mbaroni kwa madai ya kumnajisi mshukiwa aliyekuwa akizuiliwa, Tobias Nakuwa Lobolia alikamatwa Jumanne, Januari 29, kwa madai ya kumnyanyasa kimapenzi msichana wa miaka 15 aliyekuwa akizuiliwa mahabusu.
Afisa huyo wa polisi alishutumiwa kwa kumnajisi mtoto huyo ndani ya kituo cha polisi mnamo Disemba 2018, hakimu wa Kisumu aliamrisha uchunguzi kufanywa baada ya mtoto huyo kulalamika akiwa kortini na alimtambua afisa huyo baada ya maafisa hao kuletwa mbele yake.
Mshukiwa alilalamika Jumatatu, Disemab 17, 2018, alipofikishwa kortini na Hakimu akaamrisha uchunguzi kufanywa mara moja.
"Kwamba mnamo terehe 15 ya Disemba 2018 at mchana, afisa aliyetajwa aliingia katika seli ya wanawake na kumnyanyasa kimapenzi kwa kushika titi zake,"
Hata hivyo kutuo cha polisi alipokuwa akizuiliwa msichana huyo hakikutajwa, na hii ni kwa sababu za kiusalama.
Tobias sasa huenda akafunguliwa mashtaka kwa kutumia cheo chake vibaya chini ya kifungu cha sheria nambari 24 cha Sheria Kuhusu Uhalifu wa Kingono ya 2006.
Chanzo:Tuko
Social Plugin