Emmanuel Okwi kushoto na Meddie Kagere.
Taarifa ya Simba jana jumatano imeeleza kuwa maandalizi kwaajili ya safari hiyo yamekamilika na timu itasafiri kwa ndege ikipitia Nairobi hadi Kinshasa ambapo utapigwa mchezo huo.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mchezo huo utaanza saa 11:00 jioni kwa saa za DRC ambapo itakuwa ni saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Klabu inatarajiwa kurejea nchini siku ya Jumapili tayari kwa ratiba nyingine ikiwemo michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara pamoja na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Al Ahly 1, 2, 2019 nchini Misri.
Mpaka sasa Meddie Kagere ndio mfungaji bora wa ligi ya mabingwa akiwa na mabao matano katika mechi 5 hiyo ni baada ya Moataz Al-Mehdi mwenye mabao 7 timu yake ya Al Nasr kutolewa.
Emmanuel Okwi ndiye mchezaji aliyetengeneza mabao mengi zaidi ambayo ni matano.
Simba pia ndo timu iliyofunga mabao mengi zaidi kwenye michuano hiyo msimu huu ikiwa imefunga mabao 15 katika mechi 5 ilizocheza.
Chanzo:Eatv
Social Plugin