Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC WAICHAPA AFC LEOPARD 2 - 1..... YATINGA NUSU FAINALI SPORTPESA


Simba SC imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 

Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Patrick Aussems, itakutana na Bandari ya Mombasa nchini Kenya pia katika Nusu Fainali, wakati FC iliyowatoa mabingwa watetezi, Gor Mahia watamenyana na Kariobangi Sharks iliyowatoa Yanga SC. 

Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya 13 kwa shuti akimalizia krosi ya beki kutoka Brukina Faso, Zana Coulibally.

Okwi akamsetia kiungo Mzambia, Clatous Chama kuifungia Simba SC bao la pili dakika ya 48 kabla ya Vincent Oburu kuidungia AFC Leopards, zamani Abaluhya bao la kufutia machozi dakika ya 61.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Aishi Manula, Rashid Juma, Zana Coulibally, Lamine Moro, Pascal Wawa/Juuko Murshid dk46, Jonas Mkude/James Kotei dk46, Hassan Dilunga/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk76, Haruna Niyonzima, Hunlede Kissimbo/Meddie Kagere dk46, Emmanuel Okwi/Muzamil Yassin dk66 na Clatous Chama

Afc leopards: Adira Jairus, Kipyegon Isaac/Mburu Moses dakika ya 85, Oduro Isaac, Kamura Robinson, Seda Edward, Marita Brian, Whyvonne Isuza, Mukangula Eugene/Ochuka Clark dk79, Wayyeka Tutawe/Vincent Oburu dk50, Okaka Aziz/Marita Brian na Odenyi Jaffar/Sikhayi Dennis dk75.

Via>> Binzubeiry blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com