TAARIFA ZA SIRI ZA WATU 140,000 WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI ZAIBIWA NA KUVUJISHWA MTANDAONI

Taarifa za siri za watu zaidi ya 14000 waliyo na virusi vya HIV wakiwemo raia wa wageni zimeibiwa nchini Singapore na kuvujishwa mitandaoni.

Udukuzi huo unakuja miezi kadhaa baada ya rekodi za watu milioni 1.5 wa Singapore akiwemo waziri mkuu Lee Hsein Loong kuibiwa mwaka jana.

Taarifa za kibinafsi za wasingapore 5,400 na raia wa kigeni 8,800 zilizokuwa zimeorodheshwa kutoka Januari 2013 huenda zimevujishwa.

Hadi mwaka 2015, raia wa kigeni waliyo na virusi vya HIV hawakuruhusiwi kuzuru nchi hiyo japo kama watalii.

Kwa sasa, mtu yeyote anayetaka kuwa nchini humo zaidi ya siku 90 kwa ajili ya kazi, lazima afanyiwe uchunguzi wa kimatibabu kuhakikisha hana virusi vya Ukimwi.

Nani ilihusika na udukuzi huo?
Singapore ilitoa picha ya Mikhy Farrera-Brochez, raia wa Marekani anayehusishwa na kuvujisha wa taarifa za matibabu za watu binafsi

Mamlaka za nchi hiyo zinaamini aliyehusika na udukuzi huo huenda ni Mmarekani mmoja aliye na virusi vya ukimwi ambaye mpezi wake alikuwa daktari wa ngazi ya juu nchini Singapore

Mikhy Farrera-Brochez alishtakiwa na kufungwa baada ya kupatikana na kosa la ubadhirifu wa fedha na makosa mengine yanayohusiana na dawa za kulevya mwaka 2016.

Alifurushwa kutoka nchini humo mwaka uliyopita. Mpenzi wake Ler Teck Siang raia wa Singapore alishtakiwa kwa kumsaidia Farrera-Brochez kuweka taarifa za uongo katika rekodi zake za matibabu kuficha ukweli kuhusu hali yake ya HIV.

Maafisa wanasema Ler alijitolea kutoa damu yake na kuweka alam katika kitika kibandiko kuwa ni ya Farrera-Brochez ili kumwezesha kuingia nchini.

Katika taarifa, wizara ya afya ilimlaumu Ler kwa kutozingatia sera inayoongoza taarifa za watu binafsi.Singapore imeripotiwa kutafuta usaidizi wa kimataifa katika kesi

Maafisa wanasema kuwa walifahamishwa tarehe 22 mwezi huu wa Januari kuwa Farrera-Brochez huenda bado anashikilia taarifa ya sajili ya HIV.

"Sahamahani mmoja wa mfanyikazi wetu wa zamani ambaye alikua na idhini ya kufikia sajili ya taarifa binafsi za watu wenye virusi vya HIV huenda hakuzingatia mwongozo wa usalama uliyowekwa wa kushughulikia taarifa hizo"alisema waziri wa afya wa Singapore Gan Kim Yong.

Siku ya Jumatatu, maafisa wa afya walisema kuwa wamejaribu kuwasiliana na watu wote walio kwenye orodha hiyo ambao ni raia wa nchi hiyo lakini walifanikiwa kuzungumza na karibu watu 900 pekee kati ya 5,400.

Nambari ya dharura imetolewa kwa wale ambao huenda wameathiriwa na tukio hilo kupewa huduma ya ushauri nasaha.

Katibu wa wizara ya afya Chan Heng Kee amethibitisha hilo na kuongeza kuwa maafisa wanaamini Bw. Farrera-Brochez yuko ughaibuni lakini hawajui ni wapi hasa alipo.

"Kuna hofu huenda akaendelea kuvujisha taarifa hizo za siri mitandaoni," alionya Bw. Chan.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post