Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma enzi za uhai wake
Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jummane Ngoma amefariki dunia leo Jumatano Januari 30, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mtoto wa marehemu, Hassan Ngoma,akizungumza na Mwananchi amesema, “Ni kweli Mzee amefariki leo jioni hii hapa Muhimbili,” amesema Ngoma.
Hassan amesema kinachofanyika kwa sasa ni kuuhifadhi mwili wa baba yake kisha baadaye watatoa taarifa rasmi ikiwamo utaratibu wa msiba utakuwa wapi na mazishi yatafanyika wapi baada ya kikao cha familia.
Social Plugin