Mchezaji wa West Ham Andy Carroll, mwenye umri wa miaka 30, ameibuka na kuwashangaza wengi kwa kupigiwa upatu kuichukua nafasi ya mshambulizi wa Tottenham kutokana na kujeruhiwa kwa wachezaji wa timu hiyo.' (Sun)
Eden Hazard hatojiunga na Real Madrid mwezi huu lakini mchezaji huyo wa miaka 28 anataka kukataa maombi mengine yoyote na ahamie katika klabu hiyo bingwa wa Uhispania mwishoni mwa msimu. (Marca, kupitia Mirror)
Chelsea inatarajiwa kukamilisha usajili kwa mkopo wa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, mwenye umri wa miaka 31, huku naye mlinzi Emerson Palmieri, mwenye miaka 24, huenda akavuka upande wa pili kwa thamani ya £15m. (Star)Ganzalo Higuan anatarajiwa kuwasili London kesho Jumanne kukamilisha uhamisho wake kutoka Juventus kwenda Chelsea
Higuain anatarajiwa kuwasili London kesho Jumanne kukamilisha uhamisho wake kutoka Juventus kwenda Chelsea.(Express)
Kocha wa Milan Gennaro Gattuso, aliyetarajia kuwa na Higuain kwa mkopo msimu huu, anasema anakubali uamuzi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina kuondoka. (Marca)
Juventus inakaribia kufikia makubaliano ya uhamisho kwa mkopo kwa mlinzi wa Manchester United Matteo Darmian, mwenye umri wa miaka 29. (Guardian)
Mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kukataa nafasi ya uhamisho kwenda Arsenal na atasalia kwa mkopo Bayern Munich hadi 'angalau'mwisho wa msimu. (ESPN)
Chanzo : Bbc
Social Plugin