Esther Gway, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ameuawa wakati akijinasua asibakwe na anayedaiwa kufanya kitendo hicho ni fundi ujenzi.
Fundi huyo inadaiwa alikuwa akijenga nyumba ya marehemu eneo la Kariakoo katika manispaa ya Tabora.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 28, 2019 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili Januari 27, 2019 saa moja usiku.
Kamanda Nley amesema kwamba mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake muda huo na kumkaba shingo kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka huku akimkaba shingoni alisababisha kifo chake.
Na Robert Kakwesi, Mwananchi
Social Plugin