Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM -UDSM CHAPATA MAPROFESA WAPYA


Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limewathibitisha maprofesa wawili wasaidizi kuwa maprofesa kamili.


Pia baraza hilo limewathibitisha wahadhiri watano kuwa maprofesa wasaidizi, wahadhiri 13 kuwa wahadhiri waandamizi ikiwa ni pamoja na wahadhiri wasaidizi tisa kuwa wahadhiri kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kitaaluma vinavyotakiwa.

Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayeshughulikia masuala ya taaluma, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Rutinwa alisema baraza hilo la chuo hicho limewathibitisha Wineaster Anderson na Imani Sanga kuwa maprofesa chuoni hapo kutokana na kuandika machapisho mbalimbali ya kitaaluma ambayo yamewapatia alama inayohitajika.

Pia kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kitaaluma, Yusup Koleleni, Gastor Mapunda, Esther Ishengoma, Dev Jani na Ulingeta Mbamba wamekuwa maprofesa wasaidizi kutoka wahadhiri waandamizi.

Kwa mujibu wa Profesa Rutinwa, Elinaza Mjema, Evarist Magoti, Noel Lwoga, Grace Kinunda, Richard Sambaiga, Nandera Mhando, Edith Lyimo, Ernesta Mosha na Mussa Hans wamekuwa wahadhiri waandamizi.

Vilevile Juma Masele, Deusdedit Rwehumbiza, Kelefa Mwantimwa na Chacha Nyamkinda nao wamekuwa wahadhiri waandamizi.

Waliopandishwa kwa vigezo vya kitaaluma kuwa wahadhiri ni Makarius Itambu, Alfred Mulinda, Rodreck Henry, Leonia John, Michael Mashauri, Titus Ngeme, Gerald Tinali, Patrick Singogo na Cosmas Masanja.

Ametoa angalizo kuwa kupanda madaraja hayo kunaongeza idadi ya watumishi wabobevu chuoni hapo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com