Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola wakionesha mkataba wa ushirikiano wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko ya Mikoa ya Shinyanga na Mbeya baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya EfG, Penina Leveta (kulia), akiwa na viongozi wa mashirika yaliyofanya mkataba wa ushirikiano. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga.
Mtathmini Miradi wa EfG, Samora Julius, akitoa mada katika semina ya maofisa wa mashirika hayo iliyofanyika hivi karibuni.
Maofisa wa mashirika hayo wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mwezeshaji katika semina hiyo, Pentaleon Shoki akitoa mada.
Usikivu katika semina hiyo.
Mwonekano wa chumba wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika moja ya kumbi zilizopo Baraza ka Maaskofu Kurasini jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina hiyo na kusaini mkataba wa ushirikiano.
Na Dotto Mwaibale
***
Mashirika matatu yasiyo ya kiserikali yametiliana saini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kupinga ukati wa kijinsia kwenye masoko`katika mikoa ya Mbeya na Shinyanga.
Mkataba huo ulihusisha shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, Shirika la Miiko la mkoani Mbeya na Shirika la Equality for Growth (EfG) la jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kufunga semina ya siku tatu iliyowashirikisha maofisa kutoka katika mashirika hayo jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita alisema wameona waungane ili kuongeza nguvu ya kampeni ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika masoko ndani ya mikoa hiyo.
"Sisi shirika letu kwa hapa Dar es Salaam tulianza na mradi wa mpe riziki si matusi ambao ulilenga kuwalinda wanawake wafanyabiashara sokoni dhidi ya ukatili. Katika kupunguza ukatili dhidi ya wanawake katika masoko mradi huo umeweza kubadilisha mtazamo na tabia dhidi ya ukatili kwa wamawake, kuwahakikishia waathirika wa ukatili wanapata hakizao", alisema Magigita.
Alisema utafiti uliofanywa na EfG mwaka 2015 katika masoko 6 kuhusu ukatili wa kijinsia na uelewa wa sheria katika Wilaya za Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ulionesha kuwepo na ukatili dhidi ya Wanawake katika masoko ambapo asilimia 95.97 ya waliohojiwa katika masoko yote walisema kulikuwa na ukatili dhidi ya wanawake kwenye masoko yao.
Alisema zaidi ya wafanyabiashara 6500 waliweza kufikiwa na kampeni za kupinga ukatili, kampeni za kuongeza uelewa juu ya ukatili dhidi ya wanawake, sheria na haki za binadamu.
Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola alisema sasa wanakwenda kufanya kampeni kubwa ya kupinga ukaliti wa kijinsia katika Soko Kuu, Nguzonane, Kambarage, Ngokolo, Ndembezi na Majengo Mapya.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga alisema kampeni hiyo wataifanya katika masoko yote ya jijini humo.
Social Plugin