Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KANGI LUGOLA ATUMBUA VIGOGO WATANO


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewasimamisha kazi maofisa 5 wa idara ya wakimbizi wakituhumiwa kutoripoti uwepo wa nguo 1,947 zinazodaiwa ni za jeshi la Burundi, kwenye kambi za Nduta na Mtendeli zilizopo Mkoani Kigoma.


Waziri Lugola ametoa uamuzi huo leo, katika mkutano wake wa dharura na wanahabari katika ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es salaam.

Amewataja aliowasimamishwa kazi kuwa ni, Harrison Mseke (Mkurugenzi wa Huduma kwa Wakimbizi), Deusdedit Masusu (Mkurugenzai msaidizi), seleman Mzirai (Mkurugenzi msaidizi akishugulikia usalama na oparesheni), Peter Bulugu (Mkuu wa Kambi ya Nduta), na John Mwita (Mkuu wa kambi ya Mtendeli.

Aidha amesema kuwa misaada inapoingia nchini inatakiwa kukaguliwa, kwani kwa kitendo kilichofanywa ni kuhatarisha uhusiano kati ya Tanzania na Burundi.

"Leo tumekuta sare za Jeshi, kesho na keshokutwa tutakuta silaha za kivita na tunazipokea tuu bila kukagua eti ni misaada", amesema Waziri Lugola.

Disemba 31, 2018 vyombo vya dola mkoani Kigoma vilikamata nguo 1,947 zinazofanana na sare za jeshi zikiwa katika kambi za wakimbizi za Nduta na Mtendeli zilizopo mkoa wa Kigoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com