VURUGU ZA MAFUTA ZAKATISHA ZIARA YA RAIS MNANGAGWA ULAYA

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.

Rais Mnangagwa amerejea nyumbani baada ya kukatiza ziara yake nchini Urusi, kufuatia vurugu za maandamano zilizosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta.

Serikali ya Zimbabwe imekuwa ikiulaumu upinzani kutumia hali ya kupanda kwa bei ya mafuta nchini humo, kuchochea ghasia.

Aidha upinzani umesema wanachama wake wamekuwa wakichukuliwa hatua kali kama hatua ya kujibu vurugu za maandamano yanayofanywa kupinga ongezeko la mafuta.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change Nelson Chamisa amesema wengi wa wanachama wao wamekamatwa wakiwemo wabunge watano, huku afisa wake mwingine mwandamizi amejificha.

Amesema vyombo vya ulinzi vimekuwa vikikamata familia za watu majumbani mwao.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post