Michael Wambura
Aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kabla ya kufungiwa maisha na TFF na kifungo hicho kuthibitishwa na FIFA, amesema hakuna chombo chenye mamlaka ya kukaidi maamuzi ya mahakama.
Wambura amesisitiza kuwa huenda FIFA hawakupewa taarifa vizuri na TFF juu ya maamuzi ya mahakama ndio maana wakaidhinisha maamuzi yako.
"Mpaka sasa kuna kesi iliyofunguliwa Ubelgiji juu ya FIFA na walikubali kuwa maamuzi ya mahakama ya ndani ya nchi husika hayaingiliwi na FIFA kwahiyo hata kwenye hili wangepewa taarifa vizuri wasingeamua hivyo wangeacha maamuzi ya mahakama'' amesema.
Aidha Wambura amesema uamuzi aliochukua ni kuijulisha kamati ya nidhamu ya FIFA kuwa taarifa ya maamuzi waliyopelekewa na TFF tayari imeshaamuliwa na Mahakama ya ndani hivyo wao hawana mamlaka.
Kwa upande mwingine Wambura ameeleza kuwa ataipa taarifa mahakama kuwa maamuzi iliyotoa ili yafuatwe wahusika wake wamegoma kutekeleza uamuzi huo.
Wambura alifunguwa na TFF kutojihusisha na soka ambapo alifungua kesi mahakama kuu ya kupinga maamuzi hayo na mahakama ilitengua uamuzi huo wa TFF lakini TFF walikwenda mbele zaidi kwa kuijulisha FIFA ambayo nayo ilibariki maamuzi ya TFF juu ya Michael Wambura.
Social Plugin