Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ametoa siku 68 kwa halmashauri 4 za Kigoma Ujiji, Butiama, Liwale na Bahi kurejesha fedha za mradi wa elimu (Equip)zilizotumika kinyume na utaratibu.
Aidha ameelekeza mamlaka ya nidhamu kumchukulia hatua za kumuondoa kwenye nafasi yake afisa mipango wa halmashauri ya Bahi kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wake.
Halmashauri hizo ni kati ya halmashauri 8 zilizotumia fedha kinyume kiasi cha milioni 912.7 ambapo halmashauri 4 zilitekeleza agizo lake na kurejesha fedha.
"Halmashauri hizi wamenihuzunisha sana kwa kutotii maelekezo, naziagiza mpaka machi 28 mwaka huu wawe wamerejesha ili fedha hizo zitekeleze miradi iliyokusudiwa, "amesema Jafo
Mbali na hayo amemuagiza Naibu Waziri wake Mwita Waitara kuwa mkali katika kusimamia miradi ya elimu agizo ambalo Waitara ameahidi kulishughulikia.
Social Plugin