Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 12 Januari 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa kuendeleza tasnia ya mbegu nchini.
Katika Kikao kazi hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo I Jijini Dar es salaam pamoja na wadau kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu (TOSCI), na Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), vilevile walialikwa wadau kutoka Bill & Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kuongeza tija katika uzalishaji kwa kuongeza matumizi ya teknolojia ikiwemo mbegu bora.
Alisema pamoja na mambo mengine serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Magufuli imjidhartiti katika kuhakikisha kuwa nchi inajitosheleza kwa mafuta ya kula na hivyo serikali inataka mradi huo kuondoa chanagmoto katika sekta ya mbegu kwa kuzalisha mbegu za mafuta hasa za alizeti na michikichi.
Mhe Hasunga amewapongeza wadau kutoka Bill & Melinda Gates kupitia kampuni ya ushauri ya mradi wa AGRI Experience kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania kutekeleza mradi huo.
Social Plugin