Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKAZI DODOMA WAISHUKURU TBA KWA KUWAPA VIBARUA UJENZI MJI WA KISERIKALI


Shughuli za ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma Herman Tanguye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Bi.Suzana Michael anayefanya kibarua katika ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) akitoa pongezi kwa majiri wake ambaye ni TBA katika mji wa Kiserikali uliopo Mtumba Jijini Dodoma.
Bw.Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ujenzi kutoka Wakala wa Majengo (TBA) Humprey Killo akitoa tathimini ya ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika Mji wa Kiserikali uliopo Mtumba jijini Dodoma
 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)katika Mji wa Kiserikali uliopo Mtumba jijini Dodoma.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

Wakati ujenzi wa Wizara ishirini na tatu ukiendelea katika mji wa kiserikali uliopo katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma wakazi wa mji huo wamesema kuwa wameweza kunufaika kwa kupata vibarua na kujiongezea ujuzi kufuatia shughuli ya ujenzi inayoendelea.

wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya vibarua wanaofanya shughuli za ujenzi katika Wizara ya Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Bora inayojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamesema kuwa wamenufaika kutokana na ujenzi huo kwani wanaweza kuendesha maisha yao na familia zao.

Akizungumza mmoja wa vibarua hao Suzana Michael amesema kuwa amekuwa akipata ushirikianao mkubwa kutoka kwa wafanyakazi wengine wakiwemo TBA jambo ambalo hapo awali hakulitarajia.

“Nawashukuru sana TBA kwa kuweza kutujali na kuona umuhimu wanawake kuweza kufanya kazi ya ujenzi jambo ambalo kwa wengine imekuwa ni kama ndoto”amesema Suzana.

Naye Maimuna Chilemile ambaye ni mkazi wa kata ya Ipagala amesema kuwa kupitia ujenzi huo ameweza kunufaika kwa kuweza kuwasomesha watoto wake huku akiwataka wanawake wengine kuchangamkia fursa zinazoendelea za ujenzi wa mji wa kiserikali.

kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma Herman Tanguye amesema kuwa hadi sasa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za ujenzi.

“Changamoto zilikuwepo lakini hazikutuzuia kuendelea na ujenzi hivyo tulipambana mpaka sasa kila kitu kinaenda vizuri,pia vifaa vyote vinavyohitajika kwaajili ya kukamilisha ujenzi vimeshapatikana.”amesema Tanguye,

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ujenzi kutoka Wakala wa Majengo (TBA) Humprey Killo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha ndani ya muda waliopewa wa kukamilisha majengo hayo ifikapo Januari 31 wawe wamekaamilisha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com