Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MALINDI WAIPA KICHAPO YANGA...WAIONESHA MLANGO WA KUTOKEA

Mchezo wa kundi B wa kundi la Mapinduzi kati ya Yanga na Malindi umemalizika kwa Malindi kufanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Yanga, katika Uwanja wa Amaan, Visiwan Zanzibar.

Matheo Anthony alikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza kwa Yanga akiwa ndani ya18 kwa kumalizia kona kwa kisigino.


Dakika ya 41 Malindi walifanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Abdul Swamad Ali akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wa Yanga.

Dakika ya 62 Hamis Musa alimtengea pasi Juma Boluna akafanikiwa kuandika bao la pili la ushindi.

Mashabiki wa Yanga wamekaa jukwaa moja na wale wa Malindi kutokana na utamaduni wa visiwani Zanzibar tofauti na ilivyo Dar es Salaam.

Baada ya kupoteza mchezo wa leo wa kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Malindi Yanga wanayaaga mashindano rasmi.

Yanga wanaishia hatua ya makundi ya kombe la Mapinduzi baada ya kupoteza michezo yao miwili kati ya mitatu waliyocheza paka leo baada ya kufungwa na Azam FC kwa mabao 3-0 na leo na Malindi SC kwa mabao 2-1.

Mchezo wao wa mwisho utakuwa dhidi ya Jamhuri ukiwa ni kwa ajili ya kukamilisha ratiba kisha watarejea nyumbani.

Kundi B ambalo wapo kwa sasa vinara ni Azam FC wakiwa sawa na Malindi SC wenye Pointi saba wakifuatiwa na Yanga wenye Pointi tatu huku KVS wakiwa na Pointi moja kwenye kundi B.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com