Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : RMO SHINYANGA AFUNGUA WARSHA YA MFUMO WA ONLINE QIP FOLLOW UP KWA WASIMAMIZI WA HUDUMA ZA AFYA


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (RMO) ,Dkt. Rashid Mfaume.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) wameendesha Warsha ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji wa Uimarishaji Ubora katika Vituo vya kutolea huduma za afya “Online QIP Follow Up” kwa Timu ya Wasimamizi wa Huduma za afya ngazi ya halmashauri mkoani Shinyanga. 



Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Virgimark Mjini Shinyanga yamefunguliwa leo Februari 18,2019 na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume. 

Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Mfaume alisema mfumo huo Kielektroniki utawarahishia utendaji kazi hivyo kutoa huduma bora kwa wananchi. 

“Mfumo huu utaboresha utendaji kazi wetu zaidi ya ule ufuatiliaji wa kwenye makaratasi, naamini mafunzo haya yataleta tija na kuboresha huduma kwenye vituo vya afya,nataka mkawe chachu ya mabadiliko na tutafuatilia,mifumo hii inahitaji taarifa hivyo lazima tuzingatie umakini tunaweka taarifa lazima ziendane na hali halisi iliyopo kwenye maeneo yetu”,aliongeza Dkt. Mfaume. 

Aidha aliishukuru AGPAHI kwa kuwezesha mafunzo hayo na kuwaomba ushirikiano zaidi katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi. 

Naye Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mbwana Martine Degeh alisema mafunzo hayo yaliyoandaliwa na serikali kwa kushirikiana na asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia - AGPAHI AGPAHI yatasaidia katika ufuatiliaji wa taarifa kwa njia ya mtandao. 

Alisema mafunzo hayo yameshirikisha Wasimamizi wa Huduma za afya (CHMT) 31 kutoka halmashauri za Shinyanga,Manispaa ya Shinyanga,Kahama Mji,Ushetu,Msalala na Kishapu yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kufuatilia mipango kazi ya uimarishaji ubora wa huduma za afya.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume akifungua Warsha ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji wa Uimarishaji Ubora katika Vituo vya kutolea huduma za afya “Online QIP Follow Up” kwa Timu ya Wasimamizi wa Huduma za afya ngazi ya halmashauri mkoani Shinyanga. -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume akifungua Warsha ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji wa Uimarishaji Ubora katika Vituo vya kutolea huduma za afya “Online QIP Follow Up”.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mbwana Martine Degeh akielezea malengo ya Warsha ya Mfumo wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji wa Uimarishaji Ubora katika Vituo vya kutolea huduma za afya “Online QIP Follow Up”.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mbwana Martine Degeh akizungumza ukumbini.
Mratibu wa Kudhibiti na Kupambana na UKIMWI mkoa wa Shinyanga, Dkt. Peter Mlacha akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Afisa Mteknolojia Maabara kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Yohanes Silipamwambo Msigwa akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia matukio ukumbini.
Maafisa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Mshiriki wa warsha hiyo akichangia hoja ukumbini.
Washiriki wakiandika dondoo muhimu.
Washiriki wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com