Mwanaume wa Ethiopia aliyefufuka wakati wa mazishi yake miezi mwili iliyopita amefariki dunia.
Hirpha Negero alithibitishwa kufa mwezi Novemba ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akigonga jeneza.
''Nilisikia mtu akilia, nilijihisi kuishiwa na pumzi ndipo nikajaribu kujitoa katika hali hiyo, nilikua mnyonge , hata sikuweza kuzungumza," alisema Hirpha.
Baadae alisema alifanikiwa kuwaita watu, hapakua na mtu yeyote karibu.
Mchimba kaburi Etana Kena anasema watu waligutushwa na tukio hilo na wote walikimbia na kuliacha jeneza, ilibidi ajifungulie mwenyewe.
Baada kisa hicho hafla ya mazishi iligeuka kuwa sherehe.
"Nimezika zaidi ya miili 50 au 60. Sijawahi kushuhudia maajabu kama haya. Alionekana kama amefariki," Kena ambaye ni mjomba wa Hirpha alisema
Bw.Hirpha alisema kuwa aliona mahali pazuri sana wakati alipokua amepoteza fahamu, ambapo mwanamume aliyekua amevalia nguo nyeupe alimwambia rudi nyumbani.
Dkt Birra Leggese amesema huenda Hirpha alipoteza fahamu vibaya sana "deep coma".
Mchimba kaburi wa awali alimzika tena Hirpha kwa mara ya pili siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake.
''mara hii nilikua na hakika amefariki kwasababu, alishuhudia jinsi alivyougua kwa muda mrefu." alisema.
Social Plugin